×

Samia Azindua Radio Jamii, Ukatili Dhidi ya Wanawake

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Vijana wa Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Kusini Unguja baada ya kuzindua rasmi Kituo cha Redio Jamii Kati FM katika Kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja na Mradi wa Kimataifa wa Maendeleo ya Habari kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake na Wasichana (IPDC) wa UNESCO katika kijiji hicho  leo Agosti 12,2020.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 12,2020, amezindua rasmi Kituo cha Redio Jamii Kati FM katika Kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja na Mradi wa Kimataifa wa Maendeleo ya Habari kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake na Wasichana (IPDC) wa UNESCO katika kijiji hicho.

Akihutubia viongozi, watendaji na wananchi.
Akizungumza na Wananchi kupitia Redio Jamii Kati FM.
Akiondoa kitambaa kuzindua rasmi miradi hiyo.

 

Leave a Comment