MAPEMA leo Jumatano, Agosti 26, 2020, Mkurugenzi wa Benchmark Production, Ritha Paulsen, amewatambulisha majaji wapya wa msimu wa shindano la Bongo Star Search msimu wa 11.
Akiwatambulisha majaji hao leo jijini Dar es Salaam Ritha amesema anaamini uwezo wa majaji hao katika kutambua vipaji kutoka katika mikoa ambayo timu nzima itapita.
Katika kundi la majaji mwaka huu ametambulisha ingizo jipya ambao ni Ommy Dimpoz na Christian Bella huku Master J ambaye ni mmoja wa majaji wakongwe akiendelea kubaki katika nafasi yake.
Aidha, amesema mwaka huu wataanza na Mkoa wa Mbeya, Septemba 19 (Dhamira Hall), Arusha Septemba 26, Septemba (Point Zone Resort), Mwanza 3, Oktoba (Isamilo Hotel), Dodoma Oktoba 10, Oktoba (Royal Village Hotel), na mwisho wakimaliza na Dar es Salaam Oktoba 17-18 (Makumbusho ya Taifa).
