×

Bilionea Awanunulia Wanaye Magari ya Kifahari ‘Ferrari Portofino’

BILIONEA wa Nigeria amewazawadia watoto wake magari ya kifahari aina ya Ferrari Portofino. Hatua ya bilionea Femi Otedola kuwanunulia mabinti zake watau magari ya kifahari imezua gumzo katika mitandao ya kijamii nchini Nigeria.

Femi Otedola, ambaye ni tajiri mkuwa katika sekta ya mafuta, aliwazawadia mabinti zake magari aina ya Ferrari Portofino. Florence Ifeoluwa Otedola anayefahamika kwa jina maarufu kama DJ Cuppy aliweka mtandaoni picha ya magari waliyonunuliwa na baba yao siku ya Jumatano.

Aliandika baba yao amenunua magari matatu kwa watoto wake watatu- Tolani, Temi na Ifeoluwa Otedola. Habari kutoka katika taarifa za Wikipedia inaonyesha Femi Otedola ana utajiri wa zaidi ya dola bilioni 1.85 za Kimarekani.

“Baba yetu alitupeleka dukani na kutununulia kila mtu gari lake!” huo ni ujumbe uliowekwa kwenye Twitter na Temi Otedola.

Maelezo kuhusu magari hayo

Bei ya Ferrari Portofino inakadiriwa kuwa na gharama ya dola 218,750. Gari hilo si kubwa sana na muundo wake ni wa V8 lakini mwendo wake ni wa kasi sana. Cha kushangaza licha ya muonekano wake haitumii mafuta mengi.

Mwaka 1947, Enzo Ferrari alianza kuunda magari ya Ferrari katika mji wa Maranello, Italia. Ni  matajiri wakubwa tu ndiyo walio na uwezo wa kununua gari hili.

Miongoni mwa wachambuzi maarufu wa mambo, Laycon Brother, alisema, “Huu ni ufujaji wa pesa za umma! Je, Otedola anapaswa kutoa pesa kwa masikini, badala ya kufanya hivi? Natumai EFCC itachunguza jambo hili.”

 

Leave a Comment