BAADA ya kupewa ndinga na Lebo yake mpya ya Konde Gang inayomilikiwa na Harmonize, msanii Country Boy amefunguka kuwa alikuwepo kwenye lebo hiyo tangu miezi 11 nyuma kabla ya kutambulishwa kwake siku kadhaa zilizopita.
Country Boy amesema: ‘‘Mara ya mwisho kuachia kazi yangu ilikuwa ni album ya Yule boy, baada ya kuachia hiyo nilikuwa nimejipanga kwa ajili ya hii EP yangu halafu ujue mimi nilikuwepo pale Konde Gang kama miezi 11 iliyopita kabla ya kutambulishwa.’’
Pia Country Boy amewapa sifa Kundi la OMG kwa kusema huu ndiyo wakati wao wa kutamba kwani Hip Hop ya Tanzania inatakiwa kufika hadi nchi za nje, ‘‘Hasira ambayo wanayo OMG ni kubwa sana kwenye huu muziki na Hip Hop ya Tanzania, inatakiwa itoke nje kwa hiyo huu ndiyo muda wao, mfano kama Young Lunya alipata ushawishi kutoka kwa Chidi Benz.”
