×

Swizz Beatz Atoa Sababu Mondi Kuimba Kiduchu Ngoma ya Alicia

MTAYARISHAJI (producer) wa muziki wa mwanamuziki mkubwa wa Marekani, Alicia Keys, Swizz Beatz, amelazimika kutoa sababu ya kwa nini mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameimba kiduchu kwenye wimbo aliofanya na Alicia Keys wa Wasted Energy.

 

Swizz Beatz ambaye ni mume wa Alicia Keys, amekuwa akipitia na kujibu maoni mbalimbali juu ya albam mpya ya mwanamama huyo ALICIA, ambayo ndani yake anapatikana Diamond au Mondi kwenye wimbo huo alioshirikishwa na mwanamama Alicia Keys.

Baada ya Wabongo kuandika mambo mengi juu ya Mondi kusikika kiduchu kwa takriban sekunde 20 tu kwenye wimbo huo, Swizz Beatz alilazimika kufunguka kwenye moja ya komenti katika ukurasa wa Alicia Keys wa Instagram, ambapo aliandika;

“My brother for life, please let your fans know you did as you pleassed on the record and this is just part one…” Katika komenti yake hiyo, Swizz Beatz alimaanisha;

“Kaka yangu wa damu au maisha (akimaanisha Mondi), tafadhali naomba uwaambie mashabiki wako kwamba umefanya kile ambacho ulitaka kukifanya na hii ni sehemu ya kwanza tu…”

 

Baadhi ya wadau waliozungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, wamemtaka Mondi kujitokeza hadharani na kufafanua juu ya ishu hiyo, kwani Wabongo wamekuwa wakitumia lugha isiyokuwa ya staha katika kumshambulia Alicia Keys, jambo ambalo linaweza kuharibu taswira ya wasanii wa Bongo Fleva huko ughaibuni.

 

Albam hiyo yenye nyimbo 15, iliingia sokoni Ijumaa iliyopita na tayari imeanza kuweka rekodi mbalimbali kwenye mitandao inayodili na muziki duniani.

STORI: AMINA SAID, DAR

Leave a Comment