×

Shigongo Atinga Kisiwa cha Maisome Kusaka Kura

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema, Marco Makoye Agustine ‘DM’ (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa chama hicho. Wa kwanza kulia ni Mgombea Ubunge Jimbo la Buchosa kupitia tiketi ya CCM, Eric Shigongo.
..Shigongo na DM wakipanda mtumbwi kuelekea katika kisiwa cha Maisome kuzungumza na Mabalozi, Wenyeviti wa Matawi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa ajili ya kuendeleza kuboresha uimara wa chama hicho hususani kuelekea uchaguzi mkuu 2020.
Baadhi ya wakazi wa eneo la mwambao mwa ziwa Victoria waishio eneo la kijiji cha Kahunda wakipiga picha na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Sengerema, Marco Makoye Agustine ‘DM’ (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa chama hicho. Wa kwanza kulia ni Mgombea Ubunge Jimbo la Buchosa kupitia tiketi ya CCM, Eric Shigongo.
Baadhi ya wanachama wa CCM walioambatana na DM na Shigongo wakishuka kwenye mtumbwi baada ya kufika Maisome.
Mgombea Ubunge Jimbo la Buchosa, Eric Shigongo akishuka kwenye mtumbwi mara baada ya kufika katika kisiwa Cha Maisome.
Shigongo akizungumza na mmja wa wakazi wa Maisome mara baada ya kufika katika kisiwa hicho wakati akiambatana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM.

 

 

 

Leave a Comment