
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini inawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kutaka kusafirisha dawa za kulevya nje ya nchi akiwemo mfanyakazi za ndani (House Girl) wa maeneo ya Tegeta Dar.

Akizungumza na wanahabari leo Kamishina Jenerali wa mamlaka hiyo, James Wilbert Kaji amesema mnamo Septemba 17 mwaka huu mamlaka hiyo kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama walimtia mbaroni Mary Edson Mtambo (25) aliyekuwa akitaka kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroini gram 448.14

Kamishna Kaji alisema dada huyo ni mfanyakazi wa ndani maeneo ya Tegeta Jijini Dar na walipomuhoji aliwaambia alikuwa akivisafirisha kwenye nchini India kwa rafiki yake wakiume aliyemuagiza vitabu hivyo.
Kamishna huyo aliwataja wengine waliowanasa kuwa ni Joji Justin Mathew mkazi wa Kigoma Mjini aliyenaswa na kilo 16.5 za mirungi na Alex Benedicto Mtiruka mkazi wa Kasulu mkoani Kigoma aliyenaswa na kilo 32.2.

Amesema Kamishna huyo amesema wawili hao walinaswa kwenye ofisi ya shirika la Posta kitengo cha kusafirisha mizigo.
Akiwatambulisha watuhumiwa hao Kamishna Kaji amesema katika kipindi hiki cha kampeni wengi wamekuwa wakifikiri akili zao wameelekeza kwenye kampeni na kusahau jukumu la kupambana na uharifu jambo ambalo si kweli.

“Katika kipindi hiki cha kampeni wengi wamekuwa wakijidanganya kuwa akili zetu zote tumezielekeza kwenye kampeni na kusahau majukumu yetu jambo ambalo wanajidanganya.

Nawaonya wale wote wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kuwa wataishia mikononi mwa dola”. Alimaliza kusema Kamishna Kaji. HABARI/PICHA ZOTE NA RICHARD BUKOS /GPL