×

Mbatia Adai Kunusurika Kutekwa na Gari Namba za Ubalozi – Video

 

Katika hali ambayo ni ya kushangaza na ya kushtusha sana watu wanne wakiwa na gari aina ya Prado yenye namba za DFP wametaka kukatisha uhai wa M/kiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia ambae pia ni Mbunge anaetetea kiti cha ubunge katika Jimbo la Vunjo.


Mnamo Majira ya saa10 za jioni kulitoka kurupushani kali mno katika ya Msafara wa James Mbatia Pamoja na gari hiyo iliyokuwa na watu wanne ndani hali iliyozua taharuki kubwa sana kwani nikama kulikuwa na maigizo ya sinema namna magari hayo yako you kuwa ya kufukuzwa a huku James Mbatia akiwa ndani ya gari yake. Nguvu ya ziada iliongezwa na jeshi la Polisi kituo kidogo cha Himo katika hali ya haraka ya kunusuru uhai wa Kiongozi huyo kwa kuifukuza gari yenye watu hao wasio julikana na kuiblock jambo ambalo pia halikufua dafu kwani almanusura gari hiyo igonge vibaya sana gari ya OCS wa kituo cha Polisi Himo.


Polisi walilazimika kuongeza nguvu ya magari kutoka Kituo kikuu cha Polisi Moshi – Kilimanjaro ndipo walipofanikiwa kulizuia gari hilo kwa kuziba barabara zote na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu kati ya wa nne ambapo mmoja alifanikiwa kutoroka kwa kuruka Dirishani. Baada ya purukushani hizo zilizo dumu kwa zaidi ya saa2 ndipo gari hiyo ilikutwa na Mapanga,Marungu, Sime, Mikuki, Jambia na plate number nne za aina tofauti ikiwa ni pamoja na namba za ubalozi.


Watuhumiwa wamejitetea kwamba wao ni usalama wa Taifa hata hivyo mamlaka za juu za Idara hiyo zimewakana haziwafahamu. Mpka sasa watuhumiwa wanashikiliwa na jeshi la Polisi Kituo kikuu cha Polisi Moshi Kilimanjaro kwa mahojiano zaidi juu ya tukio hilo.

 

Kwa taarifa zaidi sikiliza video hapa chini:

Leave a Comment