KIKOSI cha Simba kimeifuata Tanzania Prisons ya jijini Mbeya kibabe kuhakikisha wanaibuka na pointi tatu dhidi ya wapinzani wao hao katika mchezo utakaochezwa kesho, huku ikiwakosa mastaa wanne.
Simba iliifuata Tanzania Prisons jana Jumanne kujiandaa na mchezo wa mzunguko wa sita wa Ligi Kuu Bara ikiwa na kikosi cha wachezaji 22, huku ikiwakosa nyota wake Clatous Chama, Pascal Wawa, Gerson Fraga na John Bocco kutokana na sababu tofauti tofauti.
Rekodi zinaonyesha kwa mara ya mwisho timu hizo zilipokutana msimu uliopita matokeo yalikuwa 0-0 nyumbani na ugenini, hivyo mchezo huu unatarajiwa kuwa na upinzani mkubwa.
Akizungumza na Championi Jumatano, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, amefunguka kuwa, wamejipanga kikamilifu kuweza kufanya vizuri katika mchezo huo na kudai kuwa wamesafi ri mapema ili kuweza kupata nafasi ya kufanya mazoezi.
“Kikosi kinasafi ri leo (jana) kuelekea Sumbawanga ambapo kwa sasa tupo njiani kuelekea huko na wachezaji 22, wachezaji wapo vizuri hakuna majeruhi isipokuwa walewale Bocco na Fraga ambao wanaendelea na matibabu.
“Tumekuja mapema ili kuweza kupata nafasi ya kufanya mazoezi leo na kesho na tunaamini tutafanya vizuri katika mchezo huo japo tutawakosa baadhi ya wachezaji wetu akiwemo Wawa na Chama,” alisema Rweyemamu.
Wawa, raia wa Ivory Coast na Chama, raia wa Zambia, hawajarudi nchini baada ya kusafi ri kwenda katika mataifa yao kushughulikia paspoti zao.
Stori: Khadija Mngwai, Dar es Salaam
https://globalpublishers.co.tz/ligi-ya-mabingwa-kuendelea-leo-usiku-ajax-vs-liverpool/


