Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Guinea, jana Oktoba 25, 2020 imemtangaza Rais Alpha Conde kuwa mshindi katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 18, 2020 kwa ushindi wa asilimia 59.49%.
Conde Mwenye Umri wa Miaka 82 ameshinda Kiti cha Urais kwa Muhula wa Tatu Mfululizo huku Mpinzani wake Cellou Dalein Diallo, ambaye alijitangaza mshindi wa uchaguzi wa Urais kabla ya kutangazwa rasmi kwa matokeo hayo, akipata Asilimia 33.5% ya kura.
