×

Mobetto Afunguka, Sijui Kuimba?

Msanii wa BongoFleva na filamu, Video Vixen, Mjasiriamali Hamisa Mobetto amevunja ukimya kwa kusema yeye sio mtu wa kukata tamaa kwani anaamini katika ndoto zake na hasikilizi watu wanavyosema kwamba hawezi kuimba.

 

“Mimi ni mtu ambaye huwa sikati tamaa, huwa naamini katika ‘vision’ yangu mwenyewe, naamini ndoto zako ni za kwako ambazo umepewa na Mungu, kwenye haya maisha ukisikiliza watu wanachosema hutofika, kama ulipangiwa kufika sehemu fulani utafika tu hata kama iwe vipi.

 

Aidha, Mobetto amezungumzia sababu za kuachana na meneja wake wa zamani Max Rioba amesema “Kwenye biashara na kazi kuna mikataba, kuna kazi na malengo pia, mimi na Max Rioba tuko poa kama kaka na rafiki. Kwenye maisha kila lenye mwanzo lina mwisho, kama unataka kupanuka zaidi, yeye ni muelewa na mimi pia hivyo maisha yanaendelea,” amesema Mobetto.

 

Leave a Comment