×

Marekani: Trump Amfuta kazi Waziri wa Ulinzi

RAIS Donald Trump ametangaza kumfuta kazi Waziri wa Ulinzi, Mark Esper, kwa kinachodaiwa kuwa ni wawili hao kushindwa kuelewana. Christopher Miller aliyekuwa Mkuu wa Kituo cha Ugaidi atachukua nafasi yake.

 

Esper alipishana kauli na  Trump kuhusu namna Ikulu (White House) ilivyotumia jeshi wakati wa maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi kufuatia kifo cha Mmarekani Mweusi, George Floyd.

 

Mwezi Juni, waziri huyo alisema hakukuwa na ulazima wa kutumia nguvu, jambo ambalo inadaiwa Ikulu haikupendezwa nalo na ilidhaniwa atafutwa kazi. Hata hivyo, Trump hajatoa sababu ya uamuzi wake.

 

Trump ameshindwa katika uchaguzi mkuu lakini bado ana mamlaka ya kufanya maamuzi mpaka pale Rais Mteule, Joe Biden, atakapoingia rasmi Ikulu.

Leave a Comment