×

Simba Wamfuata Ntibazonkiza

UMAFIA! Hivyo ndivyo utakavyosema baada ya kufahamika kuwa mabosi kadhaa wa Simba wamevamia nchini Burundi kufuata saini ya kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Said Ntibazonkiza ‘Saido’.

 

 

Yanga hivi karibuni ilikamilisha usajili wa kiungo huyo ambaye ni nahodha wa Timu ya Taifa ya Burundi. Jumapili iliyopita kiungo huyo aliifungia Burundi mabao mawili katika mchezo wa marudiano dhidi ya Mauritania wa kufuzu Afcon uliochezwa nyumbani kwao.

 

 

Nyota huyo aliyesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga, amefi kisha mabao matatu akicheza michezo miwili, lingine alilifunga katika mchezo wa awali uliopigwa Mauritania.

 

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, mabosi wa Simba walifi ka Burundi na kuweka kambi ya siku chache wakimsaka Ntibazonkiza kwa ajili ya kuthibitisha kama kweli amesaini mkataba kwa lengo la wao kuwazidi ujanja Yanga.

 

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa mabosi hao walifanikiwa kumpata kiungo huyo na kuzungumza naye na kukutana na majibu kuwa yeye ni mali ya Yanga mwenye mkataba wa miaka miwili ya kuichezea timu hiyo.

 

 

Aliongeza kuwa mabosi hao mara baada ya kupata majibu hayo, haraka wakageuza na kurejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuweka mipango mingine katika kusuka kikosi chao.

 

 

“Simba walikuwa hawaamini kama ni kweli Yanga wamefanikisha saini ya Ntibazokinza, hivyo wakaamua kwenda kujiridhisha kwa kumfuata kiungo huyo Burundi ili kufanya naye mazungumzo.

 

 

“Walipokwenda walifanya jitihada za kutosha kuhakikisha wanampata na kuzungumza naye, walipokutana naye akawapa majibu kuwa yeye ni mali ya Yanga mwenye mkataba wa miaka miwili.

 

 

“Kiungo huyo akamaliza kwa kuwaambia kuwa kama kweli wanamhitaji, basi wawatafute viongozi wa Yanga kwa ajili ya kuzungumza nao na wakikubali kumuachia basi atajiunga nao,” alisema mtoa taarifa huyo. Mjumbe wa Kamati ya Usajili ya Yanga ambaye ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said, hivi karibuni alisema kuwa: “Ntibazonkiza ni mali ya Yanga mwenye mkataba wa miaka miwili.

 

“Anatarajiwa kujiunga na kikosi cha Yanga mara baada ya mchezo wa marudiano dhidi ya Mauritania wa kuwania kufuzu (ambao wameucheza Novemba 15) baada ya hapo atajiunga na kambi ya pamoja tayari kwa kuanza kuichezea Yanga.

WILBERT MOLANDI NA IBRAHIM MUSSA, Dar

Leave a Comment