
BEKI wa zamani wa timu ya taifa ya Afrika Kusini na klabu ya Mamelodi Sundowns ya nchini humo, Anele Ngcongca (33) amefariki dunia asubuhi ya leo kwa ajali ya gari huko KwaZulu-Natal, Afrika Kusini.
Anele Ngcongca aliichezea timu ya Mamelodi Sundowns kwa miaka minne (2016-2020) baada ya kudumu na KRC Genk ya Ubelgiji kwa miaka tisa (2007-16).

Taarifa zinaeleza kuwa Anele alipata ajali akiwa katika gari aina ya BMW ambayo ilikuwa ikiendeshwa na mwanamke ambaye yupo mahututi. Beki huyo wa kulia hivi karibuni aliachana na mabingwa wa ligi kuu ya nchini (PSL), Mamelodi Sundowns.