
BARAZA la Mitihani la Tanzania (Necta), limetangaza watahiniwa kumi bora kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi uliofanyika Oktoba 7 na 8, 2020.
Matokeo hayo, yalitangazwa Jumamosi tarehe 21 Novemba 2020 na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk. Charles Msonde, ambayo yanaonyesha watahiniwa 833,672 kati ya 1,008,307 waliotunukiwa matokeo wamefaulu.
Aliongeza kwamba watahiniwa hao walipata alama 100 au zaidi kati ya 250 ambayo ni sawa na asilimia 82.68.
“Kati ya hao wasichana ni 430,755 ambao ni sawa na asilimia 82.24 na wavulana ni 402,917 sawa na asilimia 83.15,” alisema.
Matokeo hayo yapo hapa chini ambapo kuna mgawanyo wa wavulana kumi bora na wasichana.
