
MSANII wa Bongo Fleva anayeipeperusha vyema bendera ya Tanzania kimataifa, Nassib Abdul ‘Diamond’, ameweka rekodi baada ya kufikisha views milioni moja ndani ya saa nane tu kwenye mtandao wa Youtube.
Diamond anaikaribia rekodi ambayo inashikiliwa na msanii wa Nigeria, Davido, ambaye alifikisha views milioni moja ndani ya saa saba kupitia video yake ya FEM.