×

Gigy: Mondi Siyo Type Yangu

SEXLADY kunako anga la muziki wa Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amefunguka hana mpango wa kuwa na uhusiano na msanii mwezake Nasibu Abdul ‘Diamond’ bali wapo kwa ajili ya kazi.

 

Gigy ameyasema haya baada ya hivi karibuni kuvuma kwa tetesi kwamba anajipendekeza kwa msanii huyo.

 

“Nawashangaa sana binadamu, mnashindwa kufanya yenu kazi kumtazama Gigy yupo na nani, mbona mtateseka sana, ngoja niwaambie ukweli ni kwamba Diamond mimi siwezi kuwa naye maana siyo type yangu, mimi nina type zangu, nipo naye kwa ajili ya kazi that it,” alisema Gigy.

Leave a Comment