×

Mchungaji Anyofolewa Sikio Kisa Kufumwa na Mume wa Muumini Wake

KATIKA kipindi cha sikukuu ya Krimasi kumetokea kisanga cha kipekee katika baa moja iliyopo mjini Embu jijini Nairobi nchini Kenya baada ya mchungaji maarufu kung’atwa sikio na mume wa muumini wake alipomfumania akimkumbatia mkewe.

Duru zinaarifu kwamba mchungaji aliwahadaa waumini wake kuwa alikuwa amealikwa mjini humo kuhudhuria mkutano wa wahubiri.

Kwa mujibu wa gazeti la Taifa Leo, waumini walijitolea kwa kumchangia pesa ili afanikishe ziara yake.

“Mchungaji alichangiwa hela za usafiri na malazi na waumini wake ili ahudhurie mkutano huo. Baadhi yao waliamini kwamba kwa kumsaidia mchumbaji wao kueneza injili wangepata baraka,’’ alisema mdaku mmoja.

Taarifa za mtaani humo zinaarifu kwamba, jamaa alipanda gari hadi mjini Embu na akajitosa katika chumba kimoja cha starehe na kuagiza soda baridi!

Alimpigia simu mwanamke aliyemuumini wa kanisa lake aliyekuwa muuzaji wa mboga na matunda katika soko mjini humo ili wakutane waponde raha.

“Mchungaji alimuita muumini wake wa kike na wakaanza kupiga soga,’’ aliendelea kudokeza mtoa taarifa.

Inaarifiwa kwamba, mume wa mama huyo alipigiwa simu na jirani yake aliyewaona wakibarizi chumbani humo huku wakipapasana na kukumbatiana kimahaba.

“Mume wa mwanamke huyo alifika mara moja na akawafumania peupe wakiwa katika hali ya kutatanisha,’’ alieleza mdaku wetu.

Duru za kuaminika zinaarifu kuwa, mume wa mama huyo alimrukia mtu wa Mungu mithili ya simba mwenye njaa na kumng’ata sikio kwa hasira.

Mkewe alitoroka kupitia mlango wa nyuma alipoona mambo yamechacha.

Kwa mujibu wa mdokezi, wawili hao walitenganishwa na wahudumu wa klabu waliposikia mchungaji akipiga ukunga kwa maumivu.

Walimuonya ‘Mtu wa Mungu’ kuacha tabia ya kuwanyemelea wanawake wa watu.

Hata hivyo, alijitokeza msamaria mwema akampeleka hospitali ya kibinafsi kutibiwa.

 

Leave a Comment