×

Kocha Simba Amtaja Mbadala wa Mkude Simba SC

BIG bosi wa benchi la ufundi la Simba, Mbelgiji Sven Vandebroeck amemtaja kiungo Mzamiru Yassin kuwa ndiye ambaye atabeba mikoba ya kiungo wake Jonas Mkude leo Jumatano wakati ambao wata-pambana na FC Platinum.

 

Kocha huyo am-eongeza kuwa kiungo huyo ndiye atacheza eneo hilo baada ya ku-muandaa kwa siku kadhaa kwa ajili ya kuziba eneo hilo dhidi ya Wazimbabwe hao.Mkude amesimamishwa ndani ya kikosi hicho kutokana na suala la nidhamu ambapo anatarajiwa kulikosa pambano hilo la Ligi ya Mabingwa Afrika mbele ya FC Platinum.

 

Mbelgiji huyo amesema kwamba Mzamiru ndiye ambaye atacheza eneo hilo na kubainisha kuwa ataanza na viungo wawili wakabaji ndani ya kikosi hicho katika mchezo huo.“Katika eneo hilo ataanza Mzamiru kwa sababu amecheza hapo katika mazoezi ambayo tumefanya kwa siku kadhaa.

 

“Kwa sababu Mkude hatakuwepo na Lwanga (Thadeo) yeye hatakuwepo pia ndiyo maana yeye amekuwa na nafasi ya kuanza katika mchezo huu lakini nafikiri tutakuwa na kiungo mwingine mkabaji,” alimaliza Mbelgiji huyo.Kikosi cha Simba ambacho kinadaiwa kuwa kinaweza kuanza kwenye mchezo wa leo kipo kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti hili.

Leave a Comment