
MANCHESTER United inaweza kumsajili Jadon Sancho katika dirisha dogo la usajili mwezi huu kwa urahisi kama wakiamua kufanya hivyo.
United ilikuwa ikimuwania Sancho, 20, lakini ilishindwa kumpata kwa kuwa klabu yake ya Borussia Dortmund ilikuwa ikihitaji pauni 108m kiwango ambacho United iliona ni kikubwa.
Mara baada ya dili hilo kubwa, Sancho amekuwa hana kiwango kizuri na imeelezwa kuwa kama United itarejesha mpango wa kumsajili inaweza kuwa rahisi kwao tofauti na awali.
“United ikiamua kumsajili hakuna wa kuwazuia hata wakitaka Januari hii watampata na hata dau lake litashushwa, kwa sasa amesaliwa na mkataba wa miaka miwili na nusu,” alisema mtoa taarifa kutoka Ujerumani.