
WAZIRI wa Usafirishaji wa Zimbabwe, Joel Biggie Matiza, amefariki dunia kwa kuugua COVID 19 jana katika Hospitali ya St. Annes Harare. Matiza anakuwa waziri wa nne kufariki kwa Clovid-19 nchini humo, ambapo siku tatu zilizopita Waziri wa Mambo ya Nje, Dr. Moyo, alifariki pia kwa ugonjwa huo.
Hili imethibitishwa leo na msemaji wa serikali, Nick Mangwana. Matiza inasemekana alilazwa hospitali wiki iliyopita. Mtu huyo alikuwa ni gavana wa Jimbo la Mashonaland Mashariki na akiwa mwenyekiti wa chama tawala cha Zanu PF wa jimbo hilo.
Waziri wa Kilimo, Perrance Shiri, alifariki kutokana na ugonjwa huo mwishoni mwa mwaka jana wakati ambapo waziri wa tawala za mikoa wa jimbo la Manicaland, Ellen Gwaradzimba, Waziri wa Mambo ya Nje, Sibusiso Moyo, wote walikufa mwanzoni mwa wiki hii.
Serikali ya Zimbabwe imekumbwa na ugonjwa huu ambapo Makamu wa Rais wawili, Constantino Chiwenga na Kembo Mohadi wanasemekana wamekumbwa na ugonjwa huo.
Pia, waziri wa zamani, Aeneas Chigwedere, aliyekuwa mbunge wa chama cha Zanu, Christopher Chigumba, wote wawili walikufa wiki hii (jana) kutokana na ugonjwa huo ambao umeua karibu watu 1,000 na kuwakumba zaidi ya 30 000.