×

Simba Yasepa Na Pointi Tatu Mbele Ya Dodoma Jiji

MECHI kati ya Dodoma Jiji FC dhidi ya Simba imemalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 leo Feburuari 4, 2021 katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mabao ya Simba yalifungwa na Meddie Kagere na Benard Morrison katika vipindi vyote viwili huku bao la Dodoma Jiji lilifungwa na Cleophas Mkandala.

Baada ya mchezo, Kocha wa Simba Didier Gomes alisema muhimu kwa timu yake ilikua ni kupata alama tatu tu bila kujali timu yake ilivyocheza.

“Nimefurahia ushindi huu ambao ni muhimu kwetu kuhakikisha tunasogea juu ya msimamo, japo mchezo ulikuwa mgumu kulingana na ubora wa wapinzani wetu” alisema Gomes.

Gomes pia alisema ushindi huo umempa nguvu zaidi ya kufanya vizuri mechi inayofuata dhidi ya Azam kutokana na kuwa mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu.

Kocha wa Dodoma Jiji, Mbwana Makata alisema vijana wake walicheza kama alivyowaelekeza licha ya kufungwa.

“Wachezaji wangu wamecheza vizuri licha ya kufungwa licha ya kuwa na muda mfupi wa kujiandaa na mchezo huu” alisema Makata.

 

NI mtanange wa ligi kuu Tanzania bara kati ya DODOMA JIJI vs SIMBA SC, unachezwa leo Februari 04, katika uwanja wa Jamuhuri Dodoma… ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave a Comment