Rais Dkt. John Pombe amesema amefurahishwa na Jeshi la Magereza ambalo alikuwa amezoea kila siku kukuta mambo ya kukuudhi lakini leo amelitembelea Gereza la Isanga, na kuona sehemu ya watu walipokuwa wananyongwa, panatisha.
Magufuli amesema hayo leo Februari 4, 2021, wakati aliposhiriki Uzinduzi wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Msalato ambao umegharimu Tsh. Milioni 900, ameahidi kuwaongezea Tsh. Bilioni 2.5 ili kumalizia.
“Kama kuna siku nimefurahi ni leo, nitawaongezea Bil 2.5 ili Makao Makuu yaweze kumalizika kwa haraka, najua huo uwezo sasa Magereza mnao, Wizara ya Fedha kabla ya Wiki haijamalizika Bil 2.5 ziwe zimeshatua hapa, mmenifurahisha Milioni 900 imejenga Majengo haya yote.
“Najua Askari mtakubaliana na Mimi nilifanya vizuri kufanya mabadiliko na kumleta Meja Jen. Mzee, kwa mwendo huu hamuwezi kukwama, Mimi napenda kuona matokeo, lakini siku za nyuma ni shida.
“Hata uniform mnazozungumza Kamishna Jenerali aliyetoka ukiacha huyu wa hivi karibuni, yule wa nyuma, yeye ndiye alikuwa na tenda ya ku-supply uniform za askari kupitia mkewe, nikaweka mwingine, nae mpole, wewe utakuwa Askari uwe mpole? Nikaona nimpe Ubalozi akawe mpole huko.