
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo Februari 15, limemteua Kim Poulsen, raia wa Denmark, kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa (Taifa Stars).
Poulsen amesaini mkataba wa miaka mitatu kuifundisha Stars ambayo ipo katika kinyang’anyiro cha kutafuta nafasi ya kucheza fainali za AFCON na Kombe la Dunia ambazo zote zitafanyika 2022 nchini Cameroon na Qatar.
Kim aliwahi kuifundisha Stars kati ya mwaka 2012 na 2013 ambapo kabla ya kupewa nafasi hiyo alikuwa kocha wa timu za taifa za vijana.
Anachukua mikoba ya Etienne Ngayiragije ambaye hivi karibuni alifikia makubaliano na TFF kuvunja mkataba wake.
