×

Waislamu Watangaziwa Mfungo Siku 3

 

KATIBU wa Baraza la Maulamaa, Sheikh Hassan Chizenga, ametaka waumini wa dini ya Kiislamu nchini  kufunga kwa siku tatu kuanzia Machi 8, 2021, ili kumuomba Mungu aepushe Janga la #CoronaVirus.

 

Pamoja na Mfungo, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limeona haja ya kurejesha Dua za Kunuti katika swala zote tano hadi COVID-19 itakapotokomea.

Leave a Comment