
Shirika la Marekani la Utafiti wa Anga (NASA) limefanikiwa kukifikisha chombo chake katika Sayari ya Mirihi (Mars) na kimefanikiwa kutuma picha.
Lengo la kutuma kifaa hicho ni kuangalia uwezekano wa kuwepo uhai katika Sayari hiyo. Chombo kilichoenda kitakusanya mawe na kuyaleta duniani kwa mara ya kwanza katika historia kwa ajili ya utafiti.
Zoezi hili la kurusha chombo limegharimu takribani Tsh. Trilioni 6.9. Chombo kilichorushwa kimetua katika eneo lililoitwa Kreta ya Jezero ambalo linaaminika kuwahi kuwa na mto.
Chombo kutua katika Sayari ya Mars ni mafanikio makubwa kwa kuwa ni nusu ya Vyombo vinavyorushwa angani hufanikiwa kutua kwa usalama.