
JESHI la Marekani limetekeleza shambulio la angani lililolenga wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran nchini Syria, Pentagon imesema.
Shambulio hilo liliharibu vifaa kadhaa vilivyokuwepo katika kituo cha mpakani kilichokuwa kikitumiwa na baadhi ya wanamgambo hao.
Rais wa Marekani, Joe Biden, aliidhinisha hatua hiyo ili kujibu mashambulio ya hivi karibuni dhidi ya maafisa wa Marekani na wale wa majeshi ya muungano unoaungwa mkono na taifa hilo nchini Iraq.
