
Bondia Francis Miyeyusho amefanikiwa kumchapa kwa pointi za majaji watatu, Habibu Pengo katika pambano la usiku wa kisasi lililopigwa kwenye Uwanja wa Kinesi usiku wa kumkia leo Februari 28, 2021.
Katika pambano hilo ambalo lilikuwa la raundi nane mabondia hao walionyesha uwezo kubwa huku Miyeyusho akitumia zoefu wake kumuadabisha Pengo katika pambano hilo.

Mbali ya pambano hilo, Muhksini Swalehe ‘Alkasusu’ amefanikiwa kumtwanga kwa pointi, Haidari Mchanjo wakati Mwinyi Mzengela akimshinda kwa pointi Waziri Rosta.
Baina Mazola na Ismail Galiatano pambano lao limeisha kwa sare wakati George Bonabucha akimchakaza kwa pointi, HashimZuber.

Ibrahim Makubi ameshinda kwa pointi Idd Mbaraka huku Luckman Ngambongali akimtandika Mohamed Mpombo katika pambano hilo ambalo limedhaminiwa na +255 Global Radio, Gazeti la Spoti Xtra, Smart Gin, Kebbys Hotel, Peak Time, Dstv na Plus Tv.

Ni usiku wa ‘KISASI’ wa Desemba 27, ambaoUmewakutanisha mabondia kadhaa wa hapa nchini Tanzania, akiwemo, Mfaume Mfaume, Habibu Pengo na Wengine, katika Uwanja wa Kinesi jijini Dar.