
MFANYABIASHARA Lucas Wilium Mollel ambye pia ni Mmiliki wa Hoteli ya kifahari ya Snowcrest aliyefariki siku ya Alhamisi, Machi 11, 2021, familia Yake imethibitisha kuwa atazikwa leo Jumatatu nyumbani kwake maeneo ya kwa Mrefu.
Akizungumza na Global TV Online, mtoto wa nne wa mfanyabiashara huyo Hellen Mollel, amesema; “Mazishi ya baba yetu yatafanyika hapa nyumbani kwake Jumatatu ambapo kutakuwa ibada na maziko hapa hapa nyumbani kwake.
Hellen ambaye ni Spika wa Bunge la Vijana Afrika Mashsriki amemueleza baba yake kuwa alikuwa mpambanaji na mwenye malenmgo, na pia mpenda kufuatilia malengo yake mpaka mwisho na kuona jambo analofanya linafanikiwa kama alivyodhamiria.