
BREAKING NEWS: RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli (61) amefariki dunia majira ya saa 12 leo Jumatano, Machi 17, 2021 kwa maradhi ya moyo katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ametangaza msiba huo na kusema kuwa kutakuwa na maombolezo ya kitaifa siku 14 ambapo bendera ya Taifa itapepea nusu mlingoti.
“Tumempoteza Kiongozi wetu Shupavu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, alilazwa tarehe 6 Machi mwaka huu katika Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo la mfumo wa umeme ambalo alikua nalo kwa zaidi ya miaka 10,”- Makamu wa Rais,S amia Suluhu.