×

Jumatano Tarehe 17 Ilivyoondoka na Viongozi 3 Mashuhuri Tanzania

 

Jumatano ya tarehe 17 mwezi wa Februari na Machi mwaka 2021 hazitasahaulika masikioni mwa Watanzania ambao waliishuhudia Taifa likipoteza viongozi watatu maarufu nchini Tanzania akiwemo Rais John Magufuli.

 

Kabla ya Rais Magufuli kufariki dunia jana Jumatano Machi 17, 2021 mwezi uliopita tarehe kama hii, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad alifariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa akipatiwa matibabu.

 

 

Siku hiyo ya Februari 17 usiku, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa alitangaza kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi aliyefariki dunia saa 3 usiku katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma alikokuwa akipatiwa matibabu.

 

Viongozi wawili walizikwa kwa nyakati tofauti, Maalim Seif alizikwa Februari 18 kijijini kwake Mtambwe Pemba. Wakati Balozi Kijazi alizikwa Februari 20 katika makaburi ya Kanisa Katoliki ya Manundu wilayani Korogwe mkoani Tanga.

 

 

 

Lakini usiku wa kuamkia leo Alhamisi Machi 18, Taifa lilipata taarifa za mshtuko baada ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kuutangazia umma kuwa Rais John Magufuli amefariki dunia saa 12 jioni katika Hospitali ya Mzena jijini.


Amesema Tanzania itakuwa katika kipindi cha maombolezo kwa siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti. Wananchi watajulishwa kuhusu taratibu za maziko ya Rais John Magufuli.

Leave a Comment