
AFISA Habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli leo Aprili 9, 2021 amewakumbusha wanawachama kulipa ada zao za mwaka kuelekea kufanya mkutano wao mkuu.
Amesema mkutano huo unatarajiwa kufanyika mei ambapo watakuwa na mambo makuu mawili ambayo ni katiba na kuelekea mabadiliko ya uendeshaji wa klabu.
“Wanachama walipe ada zao huo ndio wito wangu kwao,kabla ya mkutano mkutano mkuu wa Mei,”amesema.