
WAPELESTENA 36 wameuawa na wengine 250 kujeruhiwa kufuatia shambulio la maroketi ya Israel, Kundi la Wapiganaji wa Kipalestina la Hamas limeapa kuendeleza mashambulizi dhidi ya Israel kulipiza kisasi.
Mamlaka za Israel zimeripoti kuwa kombora lililorushwa limeanguka katika bomba la mafuta na kusababisha moto mkubwa.
Wakazi wa maeneo ya Gaza wamelazimika kuondoka mapema asubuhi kukimbia athari za makombora hayo huku kukiwa na ripoti za Israel kusogeza vifaa vya kijeshi vikiwamo vifaru karibu na eneo hilo.
Wanaharakati wamemwomba Rais wa Marekani, Joe Biden kuingilia mzozo huo na kuiwajibisha Israel kwa kushambulia makazi ya watu.