×

Denti Aanguka, Afa Akijibu Swali La Hesabu

Binti mmoja wa miaka nane alianguka na kufariki aliposimama kujibu swali la hesabu katika shule ya msingi ya New View iliyopo Kayole katika jiji la Nairobi nchini Kenya.

 

Walimu walisema kuwa Jeniffer Ouma ambaye alikuwa katika darasa la pili alianguka alipokuwa akijibu swali siku ya juzi.

 

Jeniffer alipoanguka, walimu walimpumzisha katika chumba maalumu wakidhani labda angerejewa na fahamu lakini hali ilikuwa tofauti.

 

Baada ya saa moja, mwanafunzi huyo bado hakuamka na ndipo walipompeleka katika hospitali ya Mama Lucy na madaktari walipompokea na kuchukua vipimo ilibainika kuwa alikuwa amekwishafariki.

 

Maafisa wa polisi wanafanya uchunguzi ili kubaini kama kuna uhalifu wowote uliofanyika kuhusiana na kifo hicho. Mwili wa marehemu utafanyiwa uchunguzi ili kusaidia katika kesi hiyo.

Leave a Comment