Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, anatarajiwa kufungua Mashindano ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na Sekondari (UMISSETA) Juni 8, 2021 kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Akitoa taarifa kwa umma hii leo, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe amesema mashindano ya UMITASHUMTA yafanyika Juni 6 hadi 19, 2021 ambapo UMISSETA yataanza Juni 19 hadi Julai 3, 2021. Aidha, Katibu Mkuu ameongeza kuwa michezo itakayohusika ni mpira wa miguu, netiboli, mpira wa wavu, mpira wa mikono, mpira wa meza, riadha jumuishi, kwaya na ngoma.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. James Mdoe, amesema michezo inajenga afya, ubunifu, upendo, hali ya kujiamini na umoja wa kitaifa. Naye Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi amesema viongozi wa mashirikisho na vyama vya michezo ili wajionee vipaji mashindano hayo yatarushwa mubashara kupitia TV mbalimbali nchini. ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx