×

Kolabo ya Seyi Shay, Yemi Alade Yatingisha

Na Mwandishi Wetu
STAA wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Nigeria, Seyi Shay ameachia ngoma mpya, ‘Pempe’ akiwa ameshirikiana na staa mwingine mkubwa kutoka nchini humo, Yemi Alade.

Pempe ni ngoma ya kwanza kwa mwaka 2021 kutoka kwa Seyi Shay, ikiwa ni maandalizi ya mixtape yake anayotarajia kuiingiza sokoni ndani ya mwaka huu, 2021.

Prodyuza wa ngoma hiyo, ni Kel-P ambaye ndiye aliyetengeneza albamu ya Burna Boy, Africamn Giant iliyojinyakulia tuzo ya Grammy mwaka huu na ameshirikiana na Clarence Peters, dairekta mkubwa duniani ambaye ndiye aliyetengeneza video ya wimbo huo.

 

Neno Pempe, limetoholewa kutoka kwenye lugha ya mitaani nchini Nigeria, ikimaanisha msichana mrembo na tayari wimbo huo umeanza kuwa gumzo kutokana na jinsi wawili hao walivyoandika mashairi yao kwa ubunifu na ufundi wa hali ya juu.

Yemi Alade ameua zaidi kwenye wimbo huo, kutokana na mashairi yake yanayoelezea jinsi ilivyo vigumu kwa mwanamke mrembo, kuhimili mikikimikiki ya mitaani hususan kutoka kwa wanaume.

Wimbo huo umesheheni mashairi yanayobeba dhana nzima ya kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii, hususan jinsi wanaume wanavyowachukulia wanawake warembo na changamoto wanazokutana nazo wasanii wa kike.

 

KUTAZAMA KIBAO HICHO:

Leave a Comment