Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa ujenzi na uchukuzi, Mwita Waitara amesema kilio Cha Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo juu ya kuomba kupunguza tozo ya nauli kuingia na kutoka bandari ya Kanyara yamesaidia kutambua tatizo hilo kwa nchi nzima. Waitara amesema serikali imesikia kilo hicho na inafanyia kazi kupunguza tozo hizo ili kumsaidia mwananchi kupata huduma ya usafiri wa majini kwa gharama ndogo.
Aidha ameongeza kuwa tayari ameziagia mamlaka husika kufanyia kazi suala hilo na muda sio mrefu serikali itatangaza tozo ya nauli nchi nzima kwa wananchi kuingia na kutoka bandarini pamoja na mizigo yao.
“Tumpongeze Sana Mbunge wenu Eric Shigongo suala hili amepiga kelele Sana bungeni na ameisaidia serikali kujua tatizo kwa nchi nzima tayari mchakato unaendelea vizuri na tutatangaza tozo mpya nchi nzima!

