×

Global Yakabidhi Meza kwa Wakala

KAMPUNI ya Global Publishers ambao ni wachapishaji wa magazeti ya Championi, Spoti Xtra, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Uwazi na Amani imekabidhi meza tano za kuuzia magazeti kwa wakala Joshua Kijida kutoka Mbezi kwa ajili ya masoko mapya ya magazeti maeneo ya Mbezi na vitongoji vyake.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo Jumatatu, Agosti 9, 2021 katika ofisi za makao makuu ya Global Group zilizopo Sinza Mori jijini Dar es Salaam.

Juma Johanes ambaye ni Ofisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, ndiye aliyekabidhi meza hiyo kwa wakala Kijida ambapo lengo kubwa ni kuwajali na kuwarahisishia kazi wauza magazeti wetu wakati wa kuyapanga na kuyauza.

Leave a Comment