
Rais wa Tanzania, Rais Samia Suluhu akiwa Ikulu, Dar anapokea ripoti ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 2020 Katika Uchaguzi huo, Hayati John Magufuli aliibuka mshindi kwa Muhula wa Pili.
“Nawapongeza Viongozi wa Vyama vya Siasa mliohudhuria hapa inadhihirisha siasa sio uhasama, ni kweli Uchaguzi uliopita CCM ilipata ushindi mkubwa sana ila hilo halijawazuia kuja mmeonesha ukomavu mkubwa.
“Nawapongeza Viongozi wa Dini kwa kuuombea Uchaguzi wa mwaka jana, Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa kuhakikisha Uchaguzi unamalizika Salama, Vyombo vya Habari na Taasisi nyingine kwa kuhamasisha Watu kupiga kura na nawapongeza Watanzania wote kwa Uchaguzi mzuri.
“Naupongeza Uongozi wa Tume ya Uchaguzi kwa kusimamia na kuendesha vizuri Uchaguzi wa mwaka jana, hakuna shaka kwa aliyeshiriki na kushuhudia Uchaguzi wa mwaka jana atakubaliana nami kwamba ulifanyika vizuri sana tena kwa kiwango cha juu kabisa.
“Hakuna shaka kwa yeyote aliyeshiriki ama kushuhudia Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana atakubaliana nami uchaguzi ulifanyika vizuri sana tena kwa kiwango cha juu kabisa.
“Pamoja na mafanikio yaliyopatikana kwenye Uchaguzi wa mwaka jana zilikuwepo pia changamoto, ndio maana ya taarifa hii ya Uchaguzi kuwekwa hadharani ili Watu watoe mapendekezo ya kuboresha Chaguzi zijazo.
“Kuhusu ushiriki kwenye Uchaguzi, Nchi yetu ina idadi kubwa ya Wanawake kuliko Wanaume na hii inadhihirishwa na idadi ya waliojiandikisha kupiga kura mwaka jana, 50.4% ya waliojitokeza walikuwa Wanawake na Wanaume walikuwa 49.6%.
“Licha ya uwingi wa idadi ya Wanawake Tanzania, Wanawake waliojitokeza na kuteuliwa na Vyama vyao kuwania nafasi mbalimbali idadi yao ilikuwa ndogo, kati ya Wagombea 30 wa nafasi ya Urais na Wagombea Wenza, Wanawake walikuwa saba tu.
“Kwenye Ubunge katika Uchaguzi wa mwaka jana,kati ya Wagombea 1257 Wanawake walikuwa 293 na kwenye Udiwani Wanawake waliogombea walikuwa 668 kati ya 9231,nazihimiza Asasi za Kiraia kuendelea kutoa Elimu na kuhamasisha Wanawake kuwania nafasi za Uongozi kwenye Chaguzi.
“Nawahamiza Wanawake kujiamini na kujitokeza kuwania nafasi za Uongozi, natoa rai kwa Vyama vya Siasa kuwaamini Wanawake na kuwapa nafasi, Tanzania haiwezi kupata Maendeleo kwa haraka endapo zaidi ya nusu ya Wananchi ambao ni Wanawake Watabaki nyuma, washirikishwe.
“Tuziangalie Sheria zetu ili zisitumike kuwanyima Watu haki kwa masuala ya kiufundi mfano Mtu anapokosea kuandika herufi za jina lake au za Chama chake nadhani mipango ingewekwa vizuri… nilijua tu Vyama vya siasa mtashangilia, tuliwashughulikia kweli Uchaguzi 2020.
“Nilijua tu Vyama vya siasa mtashangilia, kwasababu tuliwashughulikia kweli Uchaguzi uliopita kila mlipokosea (kuandika herufi za jina au Chama) tuliwaweka pin na mkatupa fursa za kupitwa bila kupingwa, sasa tutaliangalia ila na nyie muwe makini.
“Twende tukajipange kwa Uchaguzi wa mwaka 2025, ninaposema kujipanga wale Wagombea wenzangu simaanishi kujipanga kugombea, atakayejipanga mapema Sheria zipo, ni kujipanga kwa Tume ya Uchaguzi ili iweze kufanya kazi zake vizuri.” – Rais Samia Suluhu.