×

Bunge Lataka Jerry Silaa Akamatwe

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki Maadili na Madaraka, Emmanuel Mwakasaka amesema ameomba kibali kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai cha kukamatwa kwa mbunge wa Ukonga (CCM), Jerry Silaa baada ya kutofika katika shauri lake.

 

Silaa alihojiwa mara ya kwanza na kamati hiyo Agosti 24, 2021 ambapo mwenyekiti wa kamati hiyo Mwakasaka alimtaka kurudi tena leo Alhamisi kuendelea na mahojiano lakini hajaitikia wito huo.

 

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwakasaka amesema Silaa hakutoa taarifa za kutofika kwake na kwamba kamati hiyo ilimsubiri hadi saa 8.00 mchana, hivyo wamemwomba spika kutoa kibali cha kukamatwa kwake na kufikishwa katika kikao cha kamati hiyo kesho saa 4.00 asubuhi.

 

Leave a Comment