
Huyu ni Mke wa mmoja wa Askari Polisi waliouwawa kwenye tukio la jana la kurushiana risasi lililotokea Dar es salaam karibu na Ubalozi wa Ufaransa ambapo waliuwawa Watu wanne ambao ni Askari Polisi watatu na Mlinzi mmoja wa kampuni binafsi.
“Toka tumekutana tuna miaka minne tu mpaka sasa na tumebahatika kupata Mtoto mmoja ambae sasa ana miaka miwili, taarifa za msiba nimezisikia tu kwa Watu baadae nikawa namtafuta Shemeji yangu sababu Mume wangu hakuwa anapokea simu kabisa na sio kawaida yake.
“Kauli aliyoniachia mara ya mwisho aliyoniachia wakati anaondoka anakwenda kazini kwanza aliniambia nimechoka alafu najisikia vibaya nikamwambia pole kazi njema akaniambia Mke wangu Mungu akutangulie kila unachokifanya ufanikiwe, hiyo ndio kauli aliyoiacha…”