×

Rais Samia: Nimefanya Mabadiliko ya Kimuundo – Video

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassana amesema ameamua kufanya mabadiliko ya kimuundo katika wizara mbili ili kuboresha ufanisi na utendaji wa wizara hizo.

 

Rais Samia amesema hayo leo Jumatatu, Septemba 13, 2021 wakati akizungumza kwenye hotuba yake ya kuwaapisha mawaziri aliyowateua jana.

 

“Nimeanza na mabadiliko ya kimuundo kwenye wizara mbili, iliyokuwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, sasa inabaki kuwa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo. Nimechukua Habari nimeipelekea kwenye Wizara iliyokuwa na Teknolojia ya Mawasiliano na Habari.

 

“Nimefanya hivyo ili kuifanya Wizara ya Habari na Teknoljia ya Mawasilino kutimia, yale maneno habari habari yote nimeyapeleka huko. Lakini pia ilikuwa kilio cha muda mrefu cha wanahabari kwamba ikikaa hivi itapendeza zaidi.

 

“Pia kutoa msukumo kwa Sanaa, Utamaduni na Michezo kwa sababu ilikuwa imemezwa na Habari ndio ilionekana ipo juu zaidi. Nimeona niiachie ionekane kwa uwazi zaidi sababu sanaa, utamaduni na michezo ni ajira kubwa kwa vijana wetu, inatangaza utalii wa nchi yetu,” amesema Rais Samia.

 

Leave a Comment