Katika kusherekea siku ya Simba Day, mashabiki na wapenzi wa timu ya wekundu wa msimbazi leo, wamejitokeza katika tawi la Simba Babati mjini mkoani Manyara na kufanya zoezi la kuchangia damu salama kwa lengo la kuokoa maisha.
Aidha mashabiki hao wame kuwa na matumaini makubwa na timu yao kuelekea mechi ya kirafiki ikiwa ni katika kuzindua kikosi cha Simba msimu huu.