×

Dhahabu za Isha Mashauzi Zinajenga Nyumba

MWANAMAMA mkali wa miondoko ya Taarab Bongo, Aisha Ramadhan au Isha Mashauzi anasema kuwa, vito vyake vya dhahabu alivyonavyo kwa ajili ya kutupia mwilini, thamani yake inaweza kujenga bonge la nyumba na kuweka kila kitu ndani.

 

Katika mahojiano maalum na Gazeti la IJUMAA, Isha anasema kuwa, watu wanamchukulia poa, lakini katika maisha yake anapenda kujiwekea hazina kwenye vito vya dhahabu ambavyo kwa sasa gramu moja tu ni shilingi laki moja na tisini na yeye anazo nyingi, tena zenye gramu za kutosha.

 

”Unajua watu hawaelewi kuhusiana na kujiwekea hazina kwenye vito, sasa mimi vito vya dhahabu ambavyo ninavyo, naweza kujenga nyumba nzuri sana, tena yenye kila kitu cha thamani ndani na hicho najivunia mno,” anasema Isha Mashauzi ambaye ni bosi wa Kundi la Taarab la Mashauzi Classic.

STORI: IMELDA MTEMA, DAR

Leave a Comment