
MUIGIZAJI wa Nigeria ambaye anaishi Marekani Gerogina Onuoha, amesema video chafu ya msanii Tiwa Savage kuvuja kwenye mitandao imepelekea msanii huyo kupoteza dili 4 za kampuni tofauti, amedai kuwa Savage ni msanii mzuri amebarikiwa lakini kutokana na picha hizo chafu kuvija inabidi aombe radhi .
Gerogina ameenda mbali zaidi na kutolea mfano Mwanamitindo kutoka nchini Marekani Kim Kardashian ambapo anadai aliandaa tour ya kuomba radhi kwenye vituo vya habari na vipindi ili kuokoa ‘brand’ yake aliyoitengeneza kwa zaidi ya miaka 15 .
Staa huyo amesisitiza Tiwa sio Msanii ambaye anaangaliwa Nigeria pekee ni Duniani anatakiwa kuomba radhi kwa hilo ,Tiwa Savage amepoteza dili za kampuni ikiwemo ya mtandao wa simu ya GLO, Cadibury, Pampers na nyingine nyingi .