×

Wabunge Wapya, AG Wala Kiapo Bungeni – Video

Mbunge wa Jimbo la Konde, Mohamed Said Issa (ACT-Wazalendo) ameapishwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Eliezer Feleshi amekula kiapo chake leo Jumanne mbele ya Spika wa Bunge Job Ndugai.

Dk. Eliezer Feleshi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali

Anakuwa Mwanasheria Mkuu wa 10. Feleshi aliteuliwa Septemba na Rais Samia Suluhu Hassan kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Profesa Adelardus Kilangi aliyeteuliwa kuwa balozi.

 

Feleshi ameapishwa pamoja na Wabunge wengine wawili, Emmanuel Cherehani (CCM) na Mohammed Said Issa (ACT-Wazalendo) walioshinda uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Ushetu na Konde hivi karibuni.

 

“Nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote. Nitailinda na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa sheria,” Feleshi aliomba wakati akila kiapo.

MBUNGE wa Jimbo la Ushetu Mkoa wa Shinyanga, Emanuel Peter Cherehani ameapishwa leo Novemba 2, 2021 Bungeni jijini Dodoma kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Baada ya kiapo Spika wa Bunge aliwatangazia wabunge kifo cha Mbunge wa Ngorongoro na Naibu Waziri wa Uwekezaji William Ole Nasha kilichotokea Septemba 27. Ole Nasha alifariki akiwa nyumbani kwake Jijini Dodoma na kuzikwa kijijini kwao huko Ngorongoro November 2.

Tangazo la Spika Jumatatu lilikuwa jambo la kawaida ikizingatiwa kuwa wabunge wanaketi leo kwa mara ya kwanza tangu kifo cha Mbunge mwenzao.

Leave a Comment