×

Polisi Dar: Salimisheni Silaha Zenu

IKIWA ni siku chache baada ya Waziri wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, George Simbachawene kutoa msamaha kwa wanaomiliki silaha kinyume na sheria kusalimisha silaha hizo kuanzia Novemba 1, 2021 hadi November 30, 2021.

 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum limesema silaha hizo zinapaswa kusalimishwa katika vituo vyote vya Polisi, Ofisi za Serikali za mitaa na kwa watendaji wa kata kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa 10: 00 jioni.

 

Silaha hizo ni zile zinazomilikwa kinyume cha sheria kwa sababu mbalimbali ikiwemo kuisha muda wa kibali cha umiliki au kurithi silaha iliyokuwa ikimilikiwa na aliyefariki au sababu yeyote.

 

“Jeshi la Polisi linawataka wote wanaomiliki silaha kinyume na Sheria kuhakikisha wanasalimisha silaha hizo katika muda uliotolewa na muda huo utakapomalizika msako mkali utafanyika eneo kwa eneo, nyumba kwa nyumba utafanyika ukiongozwa na taarifa za ki intelijensia.

 

“Lengo likiwa ni kuhakikisha wanaomiliki silaha kinyume na sheria wanakamatwa na hatua kali za kisheria zinachukuliwa dhidi yao,” amesema Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Jumanne Muliro. 

Leave a Comment