
DJ Sinyorita amekuwa Mtanzania pekee aliyeshinda tuzo za Afrima miongoni mwa Watanzania waliotajwa kwenye tuzo za Afrima 2021.
Sinyorita ameibuka mshindi wa tuzo kwenye Kipengele cha Dj bora wa Afrika (Best African Dj) huku akiwagalagaza wakali wengine wasiopungua tisa (9) akiwamo Dj Cuppy kutoka Ngeria, pamoja na Black Coffee (South Africa).
Kwenye tuzo hizo kwa mwaka huu Tanzania ilifanikiwa kuingiza wasanii kadhaa kwenye vipengele tofauti tofauti ikiwa ni pamoja na Harmonize, Darassa, Diamond Platnumz, Rosa ree, Zuchu, Rayvanny.