
Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametunuku Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Kijeshi wahitimu 61.
Shahada hiyo imetolewa kwa ushirikiano katika ya Chuo cha Uhasibu Arusha na Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA), Monduli.
Taasisi hizo za elimu ziliingia makubaliano ya kushirikiana mwaka 2015. Kati ya wanafunzi hao wapo walohitimu Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Kijeshi kutoka Chuo cha Kijeshi Monduli na Marubani wa ndege za Kijeshi kutoka Chuo cha Mafunzo Morogoro.