
MWANAMAMA mkali kunako Bongo Fleva, Ruby ametangaza vita kwa yeyote atakayemtongoza mpenzi wake mpya aitwaye Platform.
Ruby ambaye ni baby mama wa msanii Kusah anasema; “Yaani mpaka unakuja kumtongoza mwanaume wangu kwani hujui kama wa kwangu?
“That means shari na vita unaitaka sasa mkono wako, mkono wangu wewe kariri vimbaumbau tuna mifupa mizito sana tu, halafu mimi sijui kupiga vibao ni ngumi tu, kunja tano nikunje yangu utajua hujui….. Nyie I’m inlove. Nakupenda Platform kipenzi cha mwanangu Alyah…”
STORI; MWANDISHI WETU, DAR